Isaiah 16:8-9


8 aMashamba ya Heshboni yananyauka,
pia na mizabibu ya Sibma.
Watawala wa mataifa
wamekanyaga mizabibu iliyo mizuri sana,
ambayo ilipata kufika Yazeri
na kuenea kuelekea jangwani.
Machipukizi yake yalienea
yakafika hadi baharini.

9 bHivyo ninalia kama Yazeri aliavyo,
kwa ajili ya mizabibu ya Sibma.
Ee Heshboni, ee Eleale,
ninakulowesha kwa machozi!
Kelele za furaha kwa ajili ya tunda lako lililoiva
na kwa ajili ya mavuno zimekomeshwa.
Copyright information for SwhKC